Isaiah 30:2-5


2 awale washukao kwenda Misri
bila kutaka shauri langu,
wanaotafuta msaada wa ulinzi wa Farao,
watafutao kivuli cha Misri kwa ajili ya kimbilio.

3 bLakini ulinzi wa Farao utakuwa kwa aibu yenu,
kivuli cha Misri kitawaletea fedheha.

4 cIngawa wana maafisa katika Soani
na wajumbe wamewasili katika Hanesi,

5 dkila mmoja ataaibishwa
kwa sababu ya taifa lisilowafaa kitu,
ambalo haliwaletei msaada wala faida,
bali aibu tu na fedheha.”

Copyright information for SwhKC